Highlights

Rais Ruto ahakikishia taifa uchaguzi wa haki na salama mwaka ujao.

Na Samuel Kosgei

Rais William Ruto amejitosa katika mjadala unaoendelea kuhusu iwapo atahudumu kwa muhula mmoja au miwili, akieleza imani kuwa Kenya itafanya uchaguzi wa amani, huru na wa haki huku akiwataka Wakenya kuendelea kuzingatia umoja na maendeleo ya taifa.

Akizungumza wakati wa hafla ya maombi jijini Nairobi hii leo, Rais alisema serikali yake imejitolea kuendeleza ajenda ya mageuzi ya kitaifa kuelekea uchaguzi mkuu ujao, akisisitiza kuwa taratibu za kidemokrasia zitaheshimiwa na kulindwa.

Rais alisema masuala ya matokeo ya kisiasa, ikiwemo hatma yake ya kisiasa, yako mikononi mwa Mungu, huku akiwataka Wakenya kudumisha utulivu na kuepuka siasa za mgawanyiko.

Aidha, alikashifu juhudi zozote za kueneza migawanyiko kabla ya uchaguzi, akionya kuwa majaribio ya kuvuruga umoja wa taifa hayatofaniki

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

1 comment

comments user
Üsküdar Su Kaçağı Bulma

Üsküdar Su Kaçağı Bulma Sigorta şirketi için rapor hazırladılar, çok detaylı ve profesyoneldi.

Post Comment