Wakaazi wa Toricha, North Horr walalamikia uhaba wa maji na huduma duni za afya.
Na JB Nateleng
Wakazi wa eneo la Toricha katika wadi ya Maikona, eneo bunge la North Horr, wamelalamikia ukosefu wa maji, huduma duni za afya pamoja na hali mbaya ya barabara katika eneo hilo.
Wakiongozwa na Jarso Dabaso na Atho Roba, wakazi hao wametaja changamoto kubwa kuwa ni ukosefu wa maji kutokana na ukosefu wa visima hali ambayo imeendelea kuathiri maisha yao pamoja na mifugo kwa muda mrefu.
Pia wamelalamikia huduma duni za afya katika zahanati iliyoko katika eneo hilo wakidai kuwa muuguzi anayehudumu katika kituo hicho anaishi Maikona, jambo linalowalazimu wagonjwa kusafirishwa kwa pikipiki hadi Maikona kwa gharama ya takriban shilingi elfu saba ambazo wengi hawawezi kumudu.
Wakazi hao wamedai kuwa licha ya kuwasilisha malalamishi yao mara kadhaa kwa viongozi wao, akiwemo mwakilishi wadi pamoja na Mbunge wa North Horr, bado hawajapata msaada wowote wakiitaka serikali kushughulikia changamoto hizo haraka ili waweze kunufaika na huduma muhimu za serikali kama wananchi wengine.



Post Comment