Highlights

Mwanaume mmoja afikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa simu

Na Mwandishi wetu

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 31 amefikishwa katika mahakama ya Marsabit kwa tuhuma za wizi wa simu.

Mshukiwa Feisal Golo anadaiwa kuiba simu yenye thamani ya zaidi ya shilingi elfu 24,000 pamoja na shilingi 1,500 pesa taslimu, mnamo tarehe 23 mwezi Mei mwaka 2026 katika lokesheni ya Mountain kaunti ndogo ya Marsabit Central.

Mshukiwa alikamatwa tarehe 31 mwezi Mei na kuwasilishwa mahakamani jana Jumanne.

Hakimu Mkaazi wa mahakama ya Marsabit Edward Oboge aliagiza idara ya probesheni kuwasilisha ripoti kubaini iwapo mshukiwa anastahili kuachiliwa kwa bondi au la.

Kesi hiyo itatajwa tarehe 16 mwezi huu wa Juni.

Post Comment