Highlights

wakazi wa Kaunti ya Marsabit wapinga mapendekezo ya kufungwa kwa shule za bweni nchini

Na Abdiaziz Yusuf

Wakati mjadala kuhusu mustakabali wa shule za bweni ukiendelea nchini kufuatia visa vya wanafunzi kuchoma shule katika maeneo mbalimbali, wakazi wa Kaunti ya Marsabit wamepinga mapendekezo ya kufungwa kwa shule hizo wakisema zina mchango mkubwa katika kuboresha elimu.

Wakizungmaza na shajara wakazi hao wamesema kuwa kuimarishwa kwa huduma za ushauri nasaha, mazungumzo kati ya walimu na wanafunzi pamoja na kushughulikia malalamishi ya wanafunzi kwa wakati kunaweza kusaidia kumaliza migogoro inayochangia vurugu mashuleni.

Aidha wamesema tatizo si shule za bweni bali ni ukosefu wa maelewano wakati mwingine.

Post Comment