KWS yahimiza wananchi kuepuka uharibifu wa uzio wa mbuga ya wanyamapori ya Marsabit.
Na Caroline Waforo
Wakaazi walio karibu na mbuga ya wanyamapori ya Marsabit wamehimizwa kujiepusha na uharibifu wa ua unaozingira mbuga hiyo ili kuzua visa vya migogoro ya binadamu na wanyapori.
Wito huu umetolewa na Afisa Mkuu wa Shirika la Huduma za Wanyamapori nchini (KWS) katika ukanda wa Kaskazini Mashariki, Bakari Chongwa, ambaye amesema wakati mwingine uharibifu wa ua huchangia wanyapori kutoka mbugani na kuingia kwenye makazi ya wananchi, hali inayoweza kuhatarisha usalama wa watu na mali.
Aidha, amewataka wafugaji kuhakikisha mifugo yao inalishwa katika maeneo yaliyotengwa.
Wakati huo huo Chongwa amewaondolea hofu wakaazi wa eneo la Hulahula kufuatia milio ya risasi iliyosikika siku ya Jumanne.
Amesema kuwa maafisa wa KWS walikuwa wakiwarudisha nyati waliokuwa wametoka ndani ya mbuga.
Amefafanua kuwa hatua hiyo ilikuwa sehemu ya juhudi za kuhakikisha usalama wa wananchi na kurejesha wanyamapori hao katika mazingira yao.



Post Comment