Highlights

KWS Marsabit yawapa wafugaji wa Illeret siku 10 kuondoa mifugo mbugani.

Na Nyabande Orwa

Idara ya kuwalinda wanyamapori nchini (KWS) tawi la Marsabit imewaonya wafugaji katika eneo la Illeret dhidi ya kuingiza mifugo yao ndani ya hifadhi za wanyamapori.

Akizungumza na kituo hiki ofisini mwake, mkurugenzi msaidizi wa KWS katika eneo la uhifadhi Kaskazini , Bakari Chongwa, amesema sehemu nyingi za kaunti ya Marsabit zimepata mvua za kutosha na hivyo kuna malisho ya kutosha nje ya hifadhi. Amesema hakuna sababu ya wafugaji kupeleka mifugo mbugani.

Chongwa amesema KWS imetoa muda wa siku kumi kwa wafugaji hao kuondoa mifugo yao ndani ya hifadhi, la sivyo hatua za kisheria zitachukuliwa. Pia amekosoa baadhi ya wafugaji kwa kujenga manyatta ndani ya hifadhi kinyume cha sheria.

Wakati huo huo, Chongwa ameonya kuwa kuwepo kwa mifugo ndani ya hifadhi kunaweza kusababisha kuenea kwa magonjwa kati ya wanyamapori na mifugo wa kufugwa. Amesema hali hiyo pia huharibu mazingira kwa kupunguza malisho ya wanyamapori. Aidha, amewataka wanasiasa kutohusisha siasa katika utekelezaji wa sheria za uhifadhi.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment