Kamishna wa Kaunti ya Marsabit aonya dhidi ya uhalifu wa Wahuni
Na JB Nateleng
Kamishna wa kaunti ya Marsabit, Stanley Kamande, amesema serikali haitavumilia vitendo vya uhalifu vinavyotekelezwa na wahuni.
Kamande amewataka vijana kujiepusha na makundi ya kihalifu pamoja na wanasiasa ambao wanwatumia kuanzisha vurugu kwa mafanikio yao binafsi.
Kadhalika Kamande ameonya kuwa mtu yeyote atakayepatikana akijihusisha na vitendo vya vurugu, uharibifu wa mali, au kuvuruga amani atachukuliwa hatua kali za kisheria bila ubaguzi.
Kamande pia amewarai wakazi waliotuma maombi ya vitambulisho vya kitaifa kujitokeza na kuvichukua na kisha kujiandikisha kama wapiga kura.



Post Comment