Idara ya jinsia kaunti ya Marsabit yalaani kisa cha mauaji ya watoto wawili mapacha katika eneo la Dololo,North Horr.
January 23, 2025
Mfumo wa kutatua kesi nje ya mahakama maarufu Alternative Justice System AJS umezinduliwa rasmi leo hii katika kaunti ya Marsabit.
Uzinduzi huo umeongozwa na Jaji Mkuu Martha Koome aliyeandamana na jaji wa Mahakama kuu ya Marsabit Jesse Nyagah pamoja na Jaji wa mahakama ya Rufaa Fred Ochieng.
Akizungumza katika hafla hiyo Jaji Mkuu Koome amesema kuwa mfumo huu unatekelezwa katika jitihada za kuhakikisha kuwa wakaazi wa Marsabit wanapata nafasi ya kutatua kesi inje ya mahakama na pia kupunguza mrundiko wa kesi mahakamani.
Jaji Martha Koome amesisitiza kuwa mahakama hii ya Alternative Justice System haitashughulikia kesi zote kama anayoeleza.
Jaji Mkuu amewataka wadau wote wa mahakama kushirikiana ili kuhakikisha upatikanaji wa haki Marsabit kupitia AJS
Jaji Koome amesema mfumo huu hautashuhudia visa vyovyote vya ufisadi.
Naye Gavana wa Marsabit Muhamud Ali amesema serikali ya kaunti ya Marsabit itashirikiana na idara ya mahakama ili kufanikisha mfumo huo wa Alternative Justice System ili wakaazi wapate haki kwa haraka.
Na ili kuhakikisha kuwa wakaazi wote jimboni wanapata haki gavana Mohamud Ali ameitaka idara ya mahakama kuhakikisha kuwa huduma zake zinawafikiwa wakaazikote jimboni kutokana na ukubwa wake.
Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na kamishna wa kaunti ya Marsabit James kamau, kamanda wa polisi jimboni Leonard Kimaiyo, wakilishi wadi mbalimbali kati ya viongozi wengine.