County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Zoezi la kukagua shule zote za msingi za umaa na kibinafsi limeongoa nanga hii leo katika kaunti ya Marsabit.

Wanafunzi katika mfumo wa elimu wa CBC. Picha; Hisani

Na Isaac Waihenya,

Zoezi la kukagua shule zote za msingi za umaa na kibinafsi limeongoa nanga hii leo katika kaunti ya Marsabit.

Kwa mujibu wa msimamizi wa kiwango cha ubora wa elimu katika kaunti ya Marsabit Mumas Wanyama ni kuwa zoezi hilo ambalo linatarajiwa kuendelea hadi tarehe 20 mwezi huu linalenga kubaini iwapo shule hizo zimejiandaa vilivyo kupokea wanafunzi wa gredi ya saba ambao wanajiunga na Junior Secondary baada ya kufanya mtihani wa kitaifa.

Wanyama amesema kuwa zoezi hilo litatumika kuweka mikakati ya kuimarisha hali katika shule za msingi kuhakikisha kwamba zina kila kitu hitajika kutumiwa na wanafunzi wa Junior Secondary.

Akizungumza na Radio Jangwani  baada ya mkao na washikadau katika idara hiyo pamoja na wale wa usalama, Wanyama alisema kwamba kutokana na swala la usalama na ukubwa wa kaunti ya Marsabit shule ambazo hazitakuwa zimefikisha pia idadi ya wanafunzi 45 ambayo ndio idadi hitajika ila zitakuwa zimekithi mahitaji mengine zitaruhusiwa kuwa na Junior Secondary.

Kuhusiana na swala la wazazi kuwapeleka wanao shule za mbali Wanyama alisema.

Kwa upande wake David Saruni anayeshikilia nafasi ya kamishna wa kaunti ya Marsabit japo kwa ukaimu ambaye ameongoza mkao wa leo ametaja kuwa idara ya usalama itamarisha usalama katika kila pembe ya kaunti hii ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaedelea na masomo yao bila kutatizwa.

Wanafunzi wanaojiunga na shule za upili ngazi ya chini Junior Secondary wataripoti shuleni tarehe 30 mwezi huu wa Januari.

 

 

Subscribe to eNewsletter