County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Waziri wa maji Alice Wahome ameahidi kuwa wizari ya maji itarekebisha  visima vyote yaliyoharibika katika kaunti ya Marsabit.

Waziri wa Maji Alice Wahome pamoja na naibu gavana Solomon Gubo Riwe wakati wakati wa ziara ya kukakuga miradi ya maji jimboni Marsabit.
Picha; Radio Jangwani

Na Isaac Waihenya,

Waziri wa maji Alice Wahome ameahidi kuwa wizari ya maji itarekebisha  visima yote yaliyoharibika katika kaunti ya Marsabit ili kutatua swala la ukosefu wa maji haswa kipindi hichi cha ukame.

Akizungumza alipozuru kaunti ya Marsabit kukagua miradi ya maji,Waziri Wahome ametaja kwamba  wizara ya maji inajiza titi kuhakikisha kwamba inafikisha kikomo kero la ukosefu wa maji  hapa jimboni.

Waziri Wahome ametaja kwamba wizara yake itapea kipau mbele swala la kurekebisha vyanzo vyote vya maji jimboni na taifa nzima kabla ya kuanzisha miradi mipya.

Amekariri kwamba serekali inalenga pia kuhakikisha kwamba wananchi hapa jimboni wanapata maji ya kutosha, lengo likiwa ni kukamilisha bwawa la Badasa ambalo limetajwa kama suluhu mwafaka kwa kero la ukosefu wa maji katika jimbo la Marsabit.

Aidha waziri Wahome ameelezea kuridhiswa kwake na hatua iliyopigwa katika ukarabati wa bakuli ya maji iliyopo katika msiti wa Marsabit ambayo inatarajiwa kupunguza kero la ukosefu wa maji kwa asilimia 40 itakapokamilika.

Mradi hupo unagharimu shilingi milioni mia saba.

Kwa upande wake Naibu Gavana wa kaunti ya Marsabit Solomon Gubo Riwe, amewataka wananchi kushirikiana na idara mbalimbali ili kuhakikisha kwamba miradi ya maendeleo inakamilishwa jimboni.

Subscribe to eNewsletter