VIONGOZI WA KIDINI MARSABIT WAMEITAKA JAMII KUZINGATIA MAADILI ILI KUEPUSHA VISA VYA MAUAJI VYA WANAWAKE NCHINI
November 5, 2024
Na Isaac Waihenya,
Serekali imeitakiwa kuwachukulia hatua machifu na manaibu wao ambao wanaruhusu visa vya wizi wa mifugo kufanyika katika maeneo yao.
Kwa mujibu wa naibu mwenyeketi wa baraza la dini mbalimbali katika jimbo la Marsabit InterFaith, Sheikh Mohamed Noor ni kuwa machifu huwa na ufahamu wa kila jambo linaloendela katika kata yao na hivyo wanafaa kutoa habari muhimu kuhusu visa vya uhalifu vinavyojiri.
Ametaja kwamba visa hivyo vinachochewa na mila potovu katika jamii mbalimbali jimboni.
Akizungumza na vyombo vya habari kiongozi huyo wa kidini ametoa wito kwa wananchi kusitisha uhalifu wa aina yeyote ile, huku akiitaka idara ya usalama kuwajibika zaidi.
Kadhalika Sheikh Noor ameitaja kuwa serekali inafaa kuwarejesha maafisa wa Akiba wa KPR ili kutatua mara moja kero la ukosefu wa usalama jimboni.