WAUGUZI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAMEAPA KUENDELEA NA MGOMO WAO HADI PALE SERIKALI YA KAUNTI YA MARSABIT ITAKAPOSHUGHULIKIA MATAKWA YAO YOTE.
September 19, 2024
Na Samuel Kosgei
Washukiwa watatu wamekamatwa katika wadi ya Korr eneo bunge la Laisamis kaunti ya Marsabit baada ya kupatikana na misokoto 600 ya bangi na kilo nyingine mbili katika mkoba.
Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani chifu wa Lokesheni ya Korr Jeremiah Ntimo alisema kuwa kukamatwa kwa washukiwa hao kunafuatia taarifa kutoka kwa wananchi hatua iliyosababisha kukamatwa kwa washukuiwa hao kutoka Marsabit na Loglogo siku ya Jumapili.
Chief Ntimo aliongeza kuwa vijana hao pia walikuwa wakisaka mnunuzi wa pikipiki ambapo walikuwa tayari kuuza kwa bei ya chini.
Aliongeza kuwa tayari uchunguzi unaendelezwa ili kufahamu chanzo cha bangi hizo ila anasema huenda tayari bangi hiyo ilishauzwa katika maeneo mengine kama vile Ngurnit, Namarei na hata Korr.
Washukiwa waliokamata ni pamoja na Ali Ibrahim, Ibrae Guyo na Stephano Lekupes ambao kwa sasa wanazuiliwa na maafisa wa polisi mjini Laisamis