County Updates, Diocese of Marsabit

Uwanja wa spoti unaoendelea kujengwa katika kaunti ya Marsabit unaendelea vizuri.

Uwanja wa Marsabit.
Picha; Hisani

Na Samson Guyo,

Uwanja wa spoti unaoendelea kujengwa katika kaunti ya Marsabit unaendelea vizuri licha ya kazi hio kutofanyika kwa kasi.

Akizungumza na radio jangwani wakati kamati ya uratibu wa utekelezaji wa maendeleo ya kaunti (CDICC) ilipozuru uwanja huo jana,  meneja wa mradi huo Edwin Ogach alisema kuwa kufikia sasa wamekamilisha awamu ya pili kwenye mradi huo ikiwa ni sehemu ya watu kuketi  na kufikia sasa upo  asilimia 98%  imekamilika.

Aidha kwa mujibu wa Ogach jukwaa kuu na ambalo lilikua chini ya uangalizi wa kaunti ya marsabit haujatengezwa kufikia viwango vilivyotarajiwa.

Kulingana na Ogach sehemu ya pili iliyokamilika ilisimamiwa na idara ya taifa ya michezo (Sports Kenya) na utamalizika rasmi mwisho wa mwezi huu,aidha kwa mujibu wake ni kuwa kaunti ya marsabit imesema kuwa pesa za kukamilisha jukwaa kuu  ipo tayari japokuwa wanazidi kutafuta mwanakandarasi atakaye fanya kazi nzuri tofauti na hapo awali. Mradi huo uliidhinishwa na Rais Kenyatta mwaka wa 2017.

Subscribe to eNewsletter