County Updates, Local Bulletins

KCPE yaanza vyema katika kaunti ya Marsabit huku wanafunzi 5,994 wakikalia mtihani huo.

 

Picha;Hisani

Na Isaac Waihenya

Mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE umeanza vyema katika kaunti ya Marsabit huku wanafunzi 5,994 wakikalia mtihani huo.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa elimu kaunti ya Marsabit Titus Mbatha ni kuwa mitihani hiyo iling’oa nanga mida ya saa mbili kamili.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini mwake, Mbatha ametaja kuwa wizara ya elimu inashirikiana na ile ya Usalama kuhakikisha kuwa mitihani hiyo inaendelea bila kutatizika.

Adha mkuu huyo wa elimu wa kaunti ametaja kuwa serekali ya kaunti imepiga hatua katika ujenzi wa madarasa ya mtaala mpya wa elimu CBC huku yakitarajiwa kukamilika mwishoni mwa wiki ijayo.

 

Subscribe to eNewsletter