County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Waziri wa Fedha Ukur Yattani atishia kuwashtaki mbunge wa Saku Dido Rasso na mwakilishi wa kike katika kaunti ya Isiolo Rehema Jaldesa kwa kumchafulia jina.

Waziri Wa Fedha Ukur Yattani.
Picha; Hisani.

By Adano Sharawe,

Waziri wa Fedha Ukur Yattani amewapa muda wa siku 3 Mbunge wa Saku Dido Ali Rasso na Mwakilishi wa Wanawake katika kaunti ya Isiolo Rehema Jaldesa, kumuomba msamaha kwa njia rasmi.

Hatua hii inafuatia baada ya wawili hao kudai Yattani anachochea na kufadhili uovu unaoshuhudiwa kaunti ya Marsabit.

Hapo Jumatatu wakihutubu jijini Nairobi Rasso na Rehema walitoa wito kwa waziri wa usalama Fred Matiangi kushughulikia usalama wa jimbo hili huku wakimshutumu waziri Yatani kwa kuchochea mapigano ya kikabila.

Aidha, walitoa wito kwa rais Uhuru Kenyatta kumfuta kazi mara moja Ukur Yattani.

Kulingana na taarifa yao, Yattani anachochea jamii yake ya Gabra kutekeleza mavamizi dhidi ya jamii ya Borana, madai ambayo Yattani amekataa vikali.

Katika barua ya mahitaji yaliyotumwa kwa wabunge Rasso na Rehema kupitia mawakili wa G&A Advocates LLP, waziri Yattani anataka viongozi hao kujitokeza na kumuomba msamaha lau sivyo wafikishwe mahakamani.

Katika barua hiyo, Yattani ameshtumu Rasso na Rehema kwa kuchafua jina lake na kumfanya aonekane kama afisa wa serikali aliyekosea ofisi yake.

Subscribe to eNewsletter