VIONGOZI WA KIDINI MARSABIT WAMEITAKA JAMII KUZINGATIA MAADILI ILI KUEPUSHA VISA VYA MAUAJI VYA WANAWAKE NCHINI
November 5, 2024
By Waihenya Isaac,
Washukiwa wanne waliokamatwa katika eneo la Ele Borr katika kaunti ndogo ya Turbi,Kaunti hii ya Marsabit mnamo februari 6 mwaka huu wamefikishwa mahakamani jijini Nairobi hii leo na kushtakiwa kwa kumiliki silaha bila kibali.
Wanne hao kati yao maafisa wawili wa Kaunti ya Marsabit wamekana mashtaka dhidi yao,pamoja na shtaka la kumiliki silaha kinyume cha sheria.
Mahakama ilielezwa kuwa wanne hao Galma Jara Galgalo, Musa Dalacha, Mohammed Galmagar na Ibrahim Abduba mnamo Februari 6 wakisafiri na gari la kaunti Hii lenye nambari ya usajili 10CG016A walipatikana na silaha.
Aidha Galma Jara na Musa Dalacha pia walishtakiwa kwa kuwa hapa nchini bila kibali kwani wawili hao wanasemekana kuwa raia wa Ethiopia.
Upande wa mashtaka umeshikilia kuwa Raia hao wawili wa Ethiopia hawafai kuachiliwa kwa dhamana kwa misingi kuwa hawatahudhuria kikao cha majhakama kwa kuwa hawana makazi ya kudumu hapa nchini.