HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.
December 3, 2024
By Adano Sharawe,
Wakazi wa Turbi eneo bunge la North Horr wametoa changamoto kwa serikali kumaliza kero la utovu wa usalama unaoshuhudiwa jimboni, hasa kwenye mpaka wa Sololo na Turbi.
Wakiongozwa na Roba Bonaya, wenyeji waliozungumza na idhaa hii wameelezea kuhofia usalama wao kwani sasa majambazi wenye silaha hatari wanaonekana eneo hilo hata mchana licha ya Turbi kuwa na kituo cha polisi.
Bonaya amerejelea kisa cha hivi majuzi ambapo watu waliojihami walitekeleza mavamizi ya saa moja usiku mjini humo na kumjeruhi mzee mbele ya nyumba yake.
Siku hio hiyo mwanaume mchungaji aliuwawa na ngombe wake kuchukuliwa mchana kutoka eneo hilo.
Hiyo jana (Jumatatu) wenyeji wanadai majambazi waliwamiminia risasi kutoka kichaka kilicho karibu mida ya saa kumi na moja jioni japo hakuna aliyejeruhiwa.
Bonaya amelaumu uchochezi wa wanasiasa kwa masaibu yanayowakumba.
Bonaya anasema kwa sasa masomo ya wanafunzi yametatizika pakubwa pamoja na shughuli zao za kila siku kutokana na hofu ya mashambulizi na anahimiza serikali kuwahakikishia usalama wao.