County Updates, Diocese of Marsabit

Wafanyibiashara Katika Kaunti Ya Marsabit Walalamikia Hatua Ya Mamlaka Ya Kudhibiti Kawi Nchini EPRA Ya Kuongeza Bei Ya Mafuta.

Picha;Hisani

By Silivio Nangori,

Wafanyibiashara katika sekta ya Uchukuzi kaunti ya Marsabit walalamikia hatua ya Mamlaka ya kudhibiti kawi nchini EPRA ya kuongeza bei ya Mafuta.

Wakizungumza na Idhaa hii wafanyanyibiashara hao wamelalamikia kuongezeka kwa gharama ya Maisha wakidai kwamba itaongeza mzigokwa  mwananchi wa kawaida.

Kwa sasa wanaomba serikali kushukisha bei hiyo wakihofia hali ya gharama kupanda maradufu.

Wenyeji hao wamedai kwamba fedha wanaopewa wawakilishi wadi ungefaa kusaidia wananchi kwa maswala kama kupunguza bei ya Mafuta.

Ikumbukwe kuwa hiyo jana Mamlaka ya kudhibiti kawi nchini EPRA imetangaza kuongezeka kwa bei ya mafuta humu nchini.

Aidha baadhi wameongeza Kwamba bei ya mafuta ipunguzwe ili kuwanusuru wananchi kwa mizigo ili nao waweze kuunga mkono BBI.

Kulingana na bei hizo mpya, lita moja ya mafuta aina ya petrolio imeongezeka kwa shilingi 8.19. Lita moja ya mafuta ya diseli imeongezaka kwa shilingi 5.51 huku bei ya lita moja ya mafuta taa ikiongezeka kwa shilingi 5.32.

Mjini marsabit lita moja ya Petroli inauzwa kwa shilingi 114.84, mafuta ya diseli ikiuzwa kwa shilingi 104.25 huku mafuta taa ikiuzwa kwa shilingi 94.98.

Mjini moyale lita moja ya petrol inagarimu shilingi 114.84, mafuta ya diseli ikiuzwa kwa shilingi 105.83 huku mafuta taa ikiuzwa kwa shilingi 96.56

Lita moja ya moja ya Petroli mjini Sololo inauzwa kwa shilingi 115.47, mafuta ya diseli ikiuzwa kwa shilingi 105.88 huku mafuta taa ikiuzwa kwa shilingi 95.61.

 

Subscribe to eNewsletter