County Updates, Local Bulletins

Serekali yatakiwa kuzidisha mpango wa kusambaza chakula cha msaada kwa wenyeji wa maeneo yanayokumbwa na ukame. – Mbunge wa North Horr Chachu Ganya.

Mbunge Wa North Horr Chachu Nganya.
Picha Hisani

Na Adano Sharawe,

Mbunge wa North Horr Chachu Ganya ametoa mwito kwa serikali kuu kuzidisha mpango wa kusambaza chakula cha msaada kwa wenyeji wa maeneo yanayokumbwa na ukame.

Akiunga mkono muswada kuhusu ukame bungeni, Ganya ametaja kuwa idadi ya wananchi wanaozidi kuadhirika inazidi kuongezeka kila kuchao na kwamba serikali haina budi kuchukuwa hatua za dharura kuokoa binadamu na mifugo kaunti hizo.

Ganya anataka serikali kusambaza chakula na maji kwa vijiji na shule pamoja na kutoa fedha kwa jamii zilizoathirika.

Hata hivyo, mbunge huyo amepongeza serikali kwa juhudi zake za kuwafikia wahanga wa baa la njaa na chakula kando na fedha.

Ganya pia amepongeza serikali kwa hatua ya kuanza kuwanunua mifugo ya jamii za wafugaji kutoka kaunti kumi nchini ila anasema misaada zaidi inahitajika.

Serikali inakadiria kuwa zaidi ya watu laki moja wameathirika na ukame kaunti ya Marsabit.

Subscribe to eNewsletter