HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.
December 3, 2024
By Mark Dida,
Naibu mkurugenzi wa shirika la kuhifadhi wanyama pori kaunti ya Marsabit Robert Obran amesema kuwa wanaendelea kufanyia tafiti pembe za ndovu zilizopatikana na majangili waliotiwa mbaroni na maafisa wa kulinda msitu KWS ili mahakama kufanya maamuzi.
Hata hivyo Obran ametoa uwito kwa wakaazi wa Marsabit kuchukua jukumu la kibinafsi kuhifadhi wanyama pori katika kaunti ya Marsabit.
Aidha ametaja kuwa kuna kundi la wawindaji haramu wanaoendelea kuwinda mbuni hapa jimboni kuwa ajili ya mafuta na manyoya.
Vile vile ameomba wakaazi wa eneo hii kudumisha amani kwa ajili ya kuboresha sekta ya utalii hasa mwaka huu baada ya mlipuko ya virusi vya corona.
Amelaani mauaji ya kijamii inayoshuhudiwa kila kuchao, akisema kuwa sekta ya utalii imeathirika pakubwa kufuatia utovu wa usalama jimboni.