County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Kaunti Ya Marsabit Ni Baadhi Ya Kaunti Zilizotumia Vyema Fedha Za Umaa Katika Mwaka Wa Kifedha Wa 2019/20 Kwa Aslimia 44.1.

Picha;Hisani

By Jillo Dida Jillo,

Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko anaongoza orodha ya magavana wenye utendakazi duni kwa msingi wa namna walitumia pesa za maendeleo kulingana na taarifa ya bajeti mwaka 2021 iliyotolewa na Hazina ya Taifa.

Ripoti hiyo ilifichua kuwa kaunti zenye asilima ndogo ya rekodi ya maendeleo ni Nairobi (8.5%), Taita Taveta (18.1%), Tana River (18.4%), Samburu (18.7%) na Laikipia (19%).

Aidha wizara ya Fedha ilidai kuwa kaunti nyingi hazikutimiza sheria ya asilimia 30% ya bajeti kuhusu maendeleo kulingana na sehemu ya 107 (2) (b) ya sheria ya Matumizi ya Fedha ya Umma kulingana na sheria ya mwaka 2012 kuhusu Bajeti.

Kaunti ambazo zina asilimia kubwa ya maendeleo ni pamoja na Marsabit (44.1%), Mandera (43.4%), Kwale (39.4%), Kakamega (39.3%) na Isiolo (38.1%) zinazoongozwa na Mohamed Mohamud Ali, Ali Roba, Salim Mvurya, Wycliffe Oparanya na Mohamed Kuti mtawalia.

Wizara ya fedha pia imefichua kuwa ni kaunti 11 pekee ambazo zilifuata sheria kuhusu mishahara ambapo haitakani kuzidi 35% ya mapato.

Kaunti hizo ni Mandera, Kwale, Nakuru, Lamu, Narok, Tana River, Uasin Gishu, Kilifi, Nyandarua, Marsabit na Kericho.

Kaunti ya Kiambu imeripotiwa kuvuta mkia kwa  utendakazi duni.

Kaunti hiyo imefuatwa kwa Karibu na kaunti ya Homa Bay, Busia, Lamu na kaunti ya Kilifi inayoongozwa na Amason Kingi.

Subscribe to eNewsletter