County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Kadi 420 Za Huduma Namba Zimetolewa Kufikia Sasa Katika Kaunti Ya Marsabit.

Picha; Hisani

By Mark Dida,

Kamishna Wa Kaunti Ya Marsabit Paul Rotich Amesema Kuwa Idadi Ndogo Ya Kadi Za Huduma Namba Imewasili Kaunti Ya Marsabit Katika Awamu Ya Kwanza Ya Majaribio Uliofanyika Mwaka Wa 2019.

Akizungunza Na Kituo Hiki Kamishna Rotich Amesema Kuwa Kufikia Sasa Wameweza Kupokea Kadi 420 Kufikia Tarehe 11 Disemba Mwaka Jana Kutoka Ofisi Kuu Ya Huduma Jijini Nairobi.

Kulingana Na Kamishna Rotich Wameaza Kusambaza Kadi Hizo Za Huduma Katika Kaunti Ndogo Nne Ya Moyale, North Horr, Lasamis Na Saku.

Rotich Aidha Ametaja Kwa Awamu Ya Kwanza Itasaidia Serikali Kukabiliana Na Changamoto Ya Kusambaza Huduma Namba Na Njia Bora Ya Kutelekeza Mradi Huo.

Vile Vile Amesema Kuwa Awamu Ya Pili Ya Kujisajili Huduma Namba Inatarajiwa Kuanza Mwezi Wa Nne Mwaka Huu.

Habari Kuhusu Kadi Kuwa Tayari Na Kuchukuliwa Katika Ofisi Za Serikali Inafikia Mwananchi Kupitia Njia Ya SMS.

Subscribe to eNewsletter