County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Jamii Ya Marsabit Imetakiwa Kusitisha Mila Potovu Ya Ukeketaji Wa Wasichana.

Katibu Wa Utawala Katika Wizara Ya Elimu Mumina Bonaya.
Picha; Hisani

By Adho Isacko

Katibu Wa Utawala Katika Wizara Ya  Elimu Mumina Bonaya Ameitaka Jamii Ya Marsabit Kusitisha Mila Potovu Ya Ukeketaji Wa Wasichana.

Akizungumza Hii Leo Katika Shule Ya Msingi Ya Al-Hidaya Hapa Mjinini Marsabit Alipozuru Kutathmini Utayarifu Wa Shule  Katika Kaunti Hii, Mumina Amesema Kuwa Wazari Wananaozingatia Mila Mbali Mbali Wanafaa Pia Kuzingatia Kalenda Ya Masomo Ili Kutowazuia Wanao Kurudi Shuleni.

Aidha Mumina Amesema Kuwa Wizara Ya Elimu Itawasaidia Wanafunzi Wakike Ambao Wamepata Ujauzito Wakati Wa Likizo Ndefu Ya Corona, Ili Waweze Kuendelea Na Masomo Hadi Pale Watakapojifungua.

Kuhusiana Na Swala La Wanafunzi Wengi Kukosa Barakoa Shuleni, Mumina Amesema Kuwa Hivi Karibuni Wizara Ya Elimu Itatoa  Barakoa Kwa Shule Mbalimbali  Ili Kuwafaidi  Wasio Na Uwezo Wa Kununua.

Subscribe to eNewsletter