County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Wafanyikazi Wa Kampuni Ya Sino-Hydro Hapa Marsabit Walalamikia Dhulma Za Wachina.

Wafanyikazi Wa Kampuni Ya Ya Sino-Hydro Nje ya Afisi Za Kamishna Wa Marsabit. Picha Adho Isacko

Na Adho Isacko,

Mwakilishi  Wa Wadi Ya Marsabit Ya Kati Hassan Jarso Amewasihi Wafanyikazi Wa Kampuni Ya Majitaka Ya Sino-Hydro Kurudi Kazini Kufuatia Mgomo Wao Ambao Umeingia Siku Ya 5 Hii Leo.

Akizungumza Nao Nje Ya Afisi Ya Kamishna Wa Kaunti Hii, Jarso Amewaambia Kuwa Wameweza Kuzungumza Na Maafisa Wakuu Wa Kampuni Hiyo Na Wameamua Kuwa Malalamishi Yote Ya Wafanyikazi Hao Yataweza Kutekelezwa Haraka Iwezekanavyo.

Jarso Amesema Kuwa, Wameweka  Kamati Na Maafisa Wa Leba Ili Waweze Kupata Pesa Ambazo Wafanyikazi Wale Walikua Wamekatwa..

Pia Majeruhi Wote Ambao Wamepata Majeraha Kazini Na Wote Ambao Waliaga Dunia Kazini, Watahakikisha Kuwa Wamepata Haki Na Wanapokea Fidia

Kulingana Na Wafanyikazi Hao, Viongozi Wa Kampuni Hiyo Ambao Ni  Wachina Wamekuwa Wakiwadhulumu Kwa Miaka Miwili Sasa, Na Tangu Miaka Miwili Iliyopita Wamekuwa Wakilalamikia Dhuluma Lakini Malalamishi Yao Yameambulia Patupu.

Wanadai Kuwa Mara Kwa Mara Wanajitokeza Kuzungumza Na Wakuu Wao Lakini Hakuna Chochote Kinachofanyika.

Aidha Wafanyikazi Hao Wamesema Kuwa Suluhu Walioyaelezwa Na Mwakilishi Wadi Jarso Ni Maneno Tu Na Hawatarudi Kazini Hadi Pale Ambapo Wataona Kuna Mabadiliko.

Subscribe to eNewsletter