Local Bulletins

WANAWAKE WAJAWAZITO MARSABIT WATAKIWA KUZURU HOSPITALINI ILI KUJIKINGA NA HALI YA FISTULA

NA GRACE GUMATO

Wito umetolewa kwa wanawake wajawazito katika kaunti ya Marsabit kujitokeza na kutembelea hospitali ili kuweza kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Fistula.

Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu, Daktari wa wanawake katika kaunti ya Marsabit, Eric Simiyu ameelezea kuwa wasichana walioolewa wakiwa na umri mdogo wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa Fistula, kwani katika umri mdogo bado mifupa na tishu yake haijajengeka ipasavyo hivyo njia ya uzazi huwa mwembamba kiasi cha kumzuia mtoto kupita wakati wa kujifungua kama ilivyo katika mwanamke ndio maana mimba na ndoa za mapema hazikubaliki kamwe.

Daktari Eric anasema kuwa kesi za Fistula ambazo zimeripotiwa katika kaunti ya Marsabit ni takriban 10 kwa mwaka, pia ameongezea kuwa kuna changamoto nyingi za ugonjwa wa Fistula haswa kule mashinani kwani wanaoathirika na ugonjwa huo wanaamini kuwa watapona.

Vilevile ametaja baadhi ya dalili za ugonjwa wa Fistula akisema ni kama vile; kutoa kinyesi katika sehemu moja. Pia amesema kuwa  Fistula inaweza kutibika kwa njia ya upasuaji vilevile wanawake wameshauriwa kutembelea vituo vya afya ili kupata njia mwafaka Ya kuzuia ugonjwa huo.

Hata hivyo daktari Simuyu amewashauri wanawake wote wajawazito katika kaunti ya Marsabit, kutembelea kliniki ili waweze kuhudumiwa na pia wapate kujua afya ya mtoto sawa na hali yake.

Amewaonya dhidi ya kuchelewa kutembelea kliniki kwa wakati ili kuzuia madhara yanayotokana na kupata ugonjwa wa Fistula.

Subscribe to eNewsletter