Local Bulletins

WANANCHI MJINI MARSABIT WATALAZIMIKA KUSUBIRI ZAIDI KABLA YA HUDUMA ZA MAJI KUREJEA

NA SAMUEL KOSGEI

KAMPUNI ya kushughulikia masuala ya maji na majitaka kaunti ya Marsabit MARWASCO imesisitiza haja ya wakaazi wa mji wa Marsabit kuvumilia hatua ya maji kukatwa na kampuni hiyo wiki mbili zilizopita.

Meneja mkurugenzi wa kampuni hiyo Sora Katelo amembia shajara kuwa bado shughuli za kusafisha bwawa la Bakuli 2 bado inaendelea huku asilimia 90 ikiwa imekamilika kufikia sasa.

Sora anasema kuwa zoezi hilo la kutoa uchafu limechukua muda mrefu kinyume na walivyokusudia hivyo kuwataka wateja wao kuzidi kuwapa muda kukamilisha zoezi nzima ya kusafisha bwawa hilo.

Wiki jana Sora alikuwa amesema  kulikuwa na haja kubwa sana ya kuondoa mchanga katika bwawa hilo kutokana na gharama kubwa ya umeme na dawa inayoongezeka kutokana na kero hilo.

Alisema kuwa bwawa hilo mwisho lilisafishwa mwaka wa 1997 na hivyo aliwaomba wateja wao kuwa na subira.

 

Subscribe to eNewsletter