Local Bulletins

WAKAAZI WA MARSABIT WATAKIWA KUPEA KIPAUMBELE SUALA LA ELIMU WAKATI WA KUTOA MAONI KWENYE PUBLIC PARTICIPATION.

Na Samuel Kosgei

Wakaazi wa Marsabit wametakiwa kupea kipaumbele masuala ya elimu wakati zoezi la kutoa maoni kwenye mchakato wa kushirikisha umma yaani public participation katika wadi zao.

Afisa kwenye wizara ya elimu jimboni Marsabit Boru Godana Guyo akizungumza wakati idara yake ilipopokea viti na meza itakayotumiwa na watoto wa madarasa ya chekechekea katika shule ya Gilabaji amesema kuwa mara nyingi wananchi husahau kuipa kipaumbele masuala ya elimu kama vile madarasa na vifaa vingine vya kusomea.

Shirika lisilo la kiserikali la FH leo (Alhamisi) limeshirikiana na idara ya elimu jimboni na kuwapa wanafunzi wa shule ya Gilabaji viti 35 na meza ambayo itawafaa wanafunzi mwenye masomo yao.

John Jillo kutoka shirika la FH amesema kuwa wanalenga kushirikiana kwa karibu na idara ya elimu jimboni ili kuimarisha masomo ya watoto wa chekechea ambayo wanahitaji malezi mema kutoka kwanzia msingi wa chini.

Subscribe to eNewsletter