WAZAZI MARSABIT WAHIMIZWA KUTOWAFICHA WATOTO WALIO NA ULEMAVU WA KUPOOZA KWA UBONGO MAARUFU CELEBRAL PALSY.
November 4, 2024
NA JOHN BOSCO NATELENG
Wakazi wa Kargi Eneo bunge la Laisamis, Kaunti ya Marsabit wametaka serekali kuchunguza kisa na ambacho watu zaidi ya 500 katika eneo hilo wanaripotiwa kuugua ugonjwa wa saratani.
Wakizungumza na wanahabari, wakati wa kuanzishwa kwa mswada wa kuhoji serikali juu ya ongezeko la visa vya saratani katika eneo la Kargi na Chalbi ripoti ambayo itapelekwa katika bunge la kitaifa kwa majadiliano, Wakazi hao wamesema kuwa wengi wao wamepoteza wapendwa wao kutokana na ugonjwa wa saratani kwani wengi hawakuwa na uelewa wa ugonjwa huu.
Wakaazi wa Kargi wakizungumza na kituo hiki wamesema kuwa wamekadiria hasara wanapojikaza kuwapeleka wapendwa wao katika hospitali mbali mbali jimboni na hata nje ya kaunti hii lakini mwishowe wanabaki na majonzi ya kumpoteza mmoja wao.
Kulingana na Wakazi hawa ugonjwa huu umeletwa na zoezi la kutupwa kwa mabaki ya takataka za nyuklia katika eneo hilo.
Hivyo kurai serekali kuwafidia wale ambao wamepoteza wapendwa wao kutakana na ugonjwa huo.
Kulingana na aliyekuwa mwakilishi wadi wa eneo hilo ambaye pia aliwahi hudumu kama nesi katika hospitali ya Kargi Asumpta Galgidele ni kwamba visa hivi vya saratani vimekuwa vikiongezeka kila uchao na mara nyingi huwa vinagunduliwa katika awamu ya mwisho.
Asumpta amesema kuwa kumekuweko na uchunguzi mwingi ambao umefanywa katika eneo hilo na wakazi hawajapewa matokeo hivo kuitaka serekali kuchunguza hatua za dharura za kuhakikisha kuwa wamefanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo kikuu cha kuenea kwa ugonjwa wa saratani katika eneo hilo pana la Chalbi.