Local Bulletins

VIJANA KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAMEHIMIZWA KUWAHESHIMU WAZAZI WAO ILI KUPUNGUZA VISA VYA MIZOZO YA FAMILIA.

NA JB NATELENG

Vijana katika kaunti ya Marsabit wamehimizwa kuwaheshimu wazazi wao ili kupunguza visa vya mizozo ya familia.

Akizungumza na idhaa hii afisini mwake Padre Titus Makhoha ambaye ni Baba Paroko katika kanisa la cathedral hapa Marsabit amesikitishwa na ongezeko la visa vya vijana haswa wavulana kutoheshimu na kukosa nidhamu kwa wazazi wao haswa kina mama.

Ameelezea kuwa visa hivi ambavyo vinaripotiwa katika jamii zinatokana na malezi mbaya na hata matumzi ya mihadarati akisema kuwa ni sharti vijana wajifunze kuwa ni vyema kuheshimu wazazi wao na kusuluhisha mgogoro kwa njia mwafaka.

Wakti huo huo padre Tito amewahimiza wazazi kuwalea watoto wao katika njia nzuri ambayo inazingatia maadili mema na pia amewahimiza watoto kuheshimu wazazi wao.

 

 

 

 

Subscribe to eNewsletter