Local Bulletins

VIJANA ISIOLO WATAANDAMANA KUSHINIKIZA KUPINGA MSWADA WA FEDHA 2024

NA SAMUEL KOSGEI

Vijana kaunti ya Isiolo wamesema wako tayari kushiriki maandamano ya amani ya hapo kesho ambayo yanalenga kushinikiza wabunge kuupinga mswada wa kifedha wa 2024.

Kwa mujibu wa vijana hao walio kwenye kikundi cha GEN Z wakiongozwa na Farah Hassan ni kuwa msawada huo hauna manufaa yoyote kwa wakenya na lengo lake ni kuwakadamiza wakenya

Kauli yake ikiungwa mkono na Madina Gollo ambaye amesema kupitishwa kwa msawada huo kutaweka hatarini maisha ya watoto wasichana ambao hulemewa kununua sodo haswa katika kaunti za wafugaji

Aidha wamesema kwamba hawako tayari kuzungumuza na rais hadi mswaa huo utupiliwe mbali

Wakati uo huo wamekashifu serikali haswa idara ya usalama kwa kuteka nyara baadhi ya waandamanaji wakisema hilo ni kinyume cha sheria

Subscribe to eNewsletter