HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.
December 3, 2024
.
Na Samuel Kosgei
Mkurugenzi shirika la hifadhi ya wanyama NRT ukanda huu kaskazini ya juu Dida Fayo amesema kuwa shirika hilo linazidi kujitolea kukabili changamoto ya mabadiliko ya tabia-nchi katika kaunti ya Marsabit haswa katika maeneo ambayo kuna hifadhi za shirika hilo.
Fayo akizungumza katika hafla ya kuwapa tenki ya kuhifadhi maji wakaazi wa Songa na Badasa mjini Marsabit, amesema kuwa mashirika yote ikiwemo serikali yanafaa kuja pamoja kudhibiti matatizo hayo ya Tabianchi haswa kwa kujiandaa kuteka maji wakati wa mvua ili kusadia wakati wa kiangazi.
Shirika hilo siku ya Jumatatu liliwapa makundi ya hifadhi hiyo kutoka Songa na Badasa tenki 120 za kuhifadhi maji ya kunywa na matumizi mengine.
Wakati uo huo Fayo amesema kuwa maendeleo jimboni huenda yasipatikane iwapo wakaazi wa Saku hawatavumiliana na kuishi kwa Amani. Anasema ni jukumu la kila mmoja kuanzisha mchakato wa Amani kwani vita havisaidii.
Vile vile amesema kuwa shirika la NRT lina programu ya kueneza wito wa Amani jimboni shughuli ambayo anasema itazinduliwa hivi karibuni usajili wa timu za kuongoza Amani wa utakapokamilika. Lengo la timu hizo ni kuleta uwiano na utangamano wa jamii mbambali jimboni.