Local Bulletins

SERIKALI YAANZISHA PROGRAMU YA KUWEZESHA UWEPO WA INTANETI NA MTANDAO MAENEO YA MASHINANI KAUNTI YA MARSABIT.

Na Samuel Kosgei

Serikali imesema kuwa kwa sasa inaendesha programu ya kuwezesha uwepo wa intaneti na mtandao katika maeneo yasiyo na uwezo wa kupatikana kwa mawimbi ya mawasiliano katika kaunti ya Marsabit.

Kaimu kamishna wa Marsabit David Saruni amesema kuwa zoezi hilo la kuweka mitambo ya kuwezesha mawimbi ya mtandao inaendelea katika maeneo ya mashinani kupitia hazina iliyotengwa na mamlaka ya mawasiliano nchini CA.

Aidha kamishna Saruni akizungumza kwenye kikao kimoja mjini Marsabit amesema serikali itasuluhisha kero la kuchelewa kwa vitambulisho, vyeti vya kuzaliwa na hata vyeti vya ndoa tatizo analosema limekuwa likishuhudiwa kwa muda jimboni Marsabit.

Pia amesisitiza kuwa umeme kupitia mfumo wa kitaifa utaunganishwa kaunti ya Marsabit kama vile taifa nzima huwa limeunganishwa kupitia kusafirisha nguvu za umeme kuanzia eneo Sarima hadi mji wa Marsabit na pia kaunti ya Isiolo.

Zoezi hilo litakalogharimu shilingi bilioni 4 anasema litakamilika chini ya miaka miwili.

Subscribe to eNewsletter