Local Bulletins

KAUNTI YA MARSABIT YATAJWA KUPIGA HATUA KATIKA KUBALIANA NA UGAIDI NA ITIKADI KALI

 

Na Carol Waforo

Kaunti ya Marsabit imepiga hatua kubwa katika kukabiliana na kuziua ugaidi na itikadi kali.

Haya yamebainika katika kikao jumuishi cha kaunti ya Marsabit kilichohusisha jamii, Idara mbalimbali serikalini, mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na wanahabari kuhusiana na kukabili na kuzuia ugaidi na itikadi kali.

Ni hafla iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Act Change Transform, ACT.

Mratibu wa kikao hicho Hassan Mulata ambaye pia ni mkrugenzi mkuu wa shirika la initiative of progressive change, amesema kuwa visa vya vijana kushawishika kujiunga na makundi haramu ya kigaidi pamoja na kupata mafunzo ya itikadi kali vimepungua kwa kiasi kikubwa humu jimboni marsabit.

Mulata pia amewataka vijana kujiunga na taasisi mbalimbali ili kujiendeleza kimaisha kadhalika kujihusisha katika biashara ili kujitafutia mtaji.

Hii ni katika jitihada za kuhakikisha kuwa vijana hawashawishiki kujiunga na makundi ya kigaidi au kupata mafunzo ya itikadi kali.

Kadhalika amepongeza jamii kwa kukumbatia mazungumzo yanayohusiana na ugaidi na hatari yake. Amewataka wakaazi pia kuendelea kudumisha Amani ili kuziba mianya ya uhalifu jimboni marsabit.

Kulingana na Hassan wataendelea kutoa uhamasisho kwa vijana katika hafla mbalimbali za kijamii kama vile kutumia hafla za maombi na hata michezo zinazotarajiwa jimboni hivi karibuni.

Pia watashirikiana kwa ukaribu na vyombo vya habari ili kueneza jumbe za kuzuia ugaidi na mafunzo ya itikadi kali.

Subscribe to eNewsletter