Local Bulletins

IDARA YA WATOTO KAUNTI YA MARSABIT INAFUATILIA VISA VIWILI VYA WATOTO KUTOWEKA KATIKA MAENEO YA SOLOLO NA MOYALE.

Na Isaac Waihenya,

Idara ya watoto katika kaunti ya Marsabit inafuatilia visa viwili vya watoto kutoweka katika maeneo ya Sololo na Moyale.

Kulingani na afisa wa watoto kaunti ya Marsabit Ambrose Duba ni kuwa wazazi wa watoto hao walio kati ya umri wa miaka 14 hadi 17 walilipoti kutoweka kwa watoto hao wiki juzi katika idara hiyo na pia kwa maafisa wa usalama kwenye maeneo yao.

Akizungumza na Meza ya habari ya Radio Jangwani ofisini mwake, Duba aliwataka wazazi kuwa makini na wanao kwani wanaweza lengwa na makundi yenye mafunzo ya itikadi kali.

Hata hivyo Duba aliwataka wazazi kufuatilia mienendo ya wanao haswa wanapotoka nyumbani kwenda shuleni huku akisema kwamba wengine wao hushia mitaani kuranadaranda jambo ambalo pia wanalifuatilia ili kuhakikisha kuwa watoto wanaorandaranda mjini Marsabit wanarejeshwa shuleni.

Kadhalika Duba aliwarai wazazi katika kaunti ya Marsabit kutowaficha watoto walio na ulemavu na badala yake kuwatoa ili wapate misaada mbalimbali kutoka kwa serekali.

 

Subscribe to eNewsletter