HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.
December 3, 2024
NA ISAAC WAIHENYA
Msimamizi wa zoezi la kusambaza chanjo katika kaunti ndogo ya Laisamis kaunti ya Marsabit Bi. Naomi Lentoror amekanusha madai ya kukosekana kwa chanjo mbalimbali katika wadi ya Loiyangalani.
Akizungumza na Idhaa hii kwa njia ya simu,Bi. Lentoror ametaja kwamba idara hiyo ilisambaza chanjo katika vituo vyote vya afya kwenye kaunti ndogo hiyo wiki mbili zilizopita, na kwa sasa idadi iliyosalia bado inatosha.
Aidha Bi. Lentoror ameahidi kuwa idara hiyo itasambaza chanzo nyingine iwapo zilizopo katika vituo zitatumika zote kwani kuna idadi ya kutosha ya chanjo katika bohari la kaunti.
Ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanao wanapata chanjo mbalimbali zinazotolewa kwa watoto kwa faida ya afya yao.