Local Bulletins

Gavana Mohamud Ali aendeleza cheche za maneno dhidi ya seneta Chute

Na Samuel Kosgei

GAVANA wa kaunti ya Marsabit Mohamud Ali ameendeleza cheche za maneno dhidi ya seneta wa Marsabit Mohamed Chute akisema kuwa asitishe shutuma za urongo dhidi ya serikali yake.

Gavana Ali akizungumza Ijumaa alipokuwa akizindua jengo jipya la bweni la wanafunzi katika shule ya wasichana ya Moi Girls alikana kuwa serikali imeharibu pesa za umma kama alivyodai seneta Chute.

Alisema kuwa uongozi wake tayari imetoa majibu yote ya maswali yaliyoulizwa na bunge la seneti.

“Yale maneneo anauliza uliza yote tutayajibu, juzi tuliulizwa mambo ya internship pamoja na MCAs weyu hapa. Tulifanya makosa tukaweka pesa ya internship kwa development na hiyo tunakubali lawama” alisema gavana Ali

Gavana Ali wakati huo huo alimtaka Seneta amkome bila kumfuatilia kwenye masuala uongozi akidai kuwa madai yake seneta hayana mashiko wala uzito kwani masuala yote aliyoibuliwa yamejibiwa ipaswavyo.

Subscribe to eNewsletter