Local Bulletins

Afueni kwa wakaazi wa Laisamis baada ya kampuni ya windpower kufungua maabara jipya Loglogo

Na Samuel Kosgei

Wakaazi wa eneo bunge la Laisamis wana kila sababu ya kutabasamu baada ya maabara ya kisasa kufunguliwa katika hospitali ya Loglogo.

Maabara hiyo imejengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya kuzalisha umeme kutumia upepo Lake Turkana Wind Power kupitia mpango wake wa Winds of Change ikishirikiana na Kampuni ya huduma za ndege ya Boscovik air charters limited.

Maabara hiyo imegarimu Winds of Change zaidi ya shillingi millioni 15.

Akikabidhi maabara hiyo kwa serikali ya kaunti ya Marsabit, Mkurugenzi Mkuu wa Lake Turkana Wind Power Max Schiff amesema moja kati ya malengo makuu ya kampuni yake kando na elimu na maji ni kuleta huduma bora za Afya karibu na wenyeji.

Max ameongeza kuwa sasa wakazi wa Kaunti ndogo ya Laisamis hawatalazimika kusafiri mwendo mrefu kutafuta huduma ya vipimo.

Ni kauli ambayo imepigwa jeki na afisa mkuu wa mipango wa Lake Turkana Wind Power Job Lengoiyap.

Lengoiyap ameongeza kuwa wakaazi wa Kaunti ndogo ya Laisamis wamekuwa wakilazimika kusafiri hadi aidha hospitali ya rufaa ya Marsabit au hospitali ya rufaa ya Isiolo.

Aidha Lengoiyap amesema maabara hiyo itafanikisha utafiti ni wa magonjwa sugu kama vile Kalazaa ambayo yamekuwa yakiwahangaisha wakaazi wa Kaunti ndogo ya Laisamis.

Vile vile Lengoiyap ametoa changamoto kwa serikali ya kaunti ya Marsabit kuwatuma haraka wataalamu wa Afya Katika maabara hayo.

Subscribe to eNewsletter