Local Bulletins

TAMASHA YA MUZIKI IMENG’OA NANGA KATIKA SHULE YA UPILI WA WAVULANA YA MARSABIT BOYS.

TALASO HUQA

Tamasha ya muziki imeng’oa nanga katika shule ya upili wa wavulana ya Marsabit Boys.
Shule ambazo zimehudhuria ni shule 4 za msingi na shule 14 za upili kutoka kaunti ya Marsabit.
Akizungumza na idhaa hii mwenyekiti wa shindano la muziki kaunti ya Marsabit Madina Harme Oche amesema kuwa muziki inasaidia wanafunzi kuendeleza talanta zao.
Madina ameongeza na kusema kuwa mziki hapo awali haikuwa lazima lakini kwa sasa katika mtaala mpya ya masomo CBC imekuwa ni lazima.

Pia Madina amehimiza shule ambazo hazijajihusisha pia ziweze kujihusisha ilikusaidia kutambua talanta za wanafunzi hao kwenye muziki.
Wakti uo huo ameshukuru serikali na benki ya equity kwa kushirikiana kuwasaidia kufanikisha tamasha hiyo.
Amesema pia shule ambazo zitashinda kwenye tamasha ya mziki katika kaunti ya Marsabit wataenda kwenye mashindano mengine katika kaunti ya Machakos.

Subscribe to eNewsletter