HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.
December 3, 2024
NA GRACE GUMATO
Wakaazi wa Boru Haro eneo bunge la Saku kaunti hii ya Marsabit wamelalamikia barabara mbovu ambayo haijakarabatiwa kwa kipindi cha miaka minne iliyopita.
Jarso Duba ambaye ni mzee wa kijiji katika eneo la Boru Haro amesema kuwa tangu mvua kunyesha mwezi uliopita barabara zimeharibika kiasi cha kwamba imetatiza wakaazi kuenda mji wa Marsabit akisema bei ya bidhaa na hata nauli ya kusafiri imekuwa ghali mno.
Wakazi Pia hao wamelalamikia uhaba wa maji wakisema wanatembea kilomita kadhaa kutafuta maji huku wakiomba serikali ya kaunti na serikali kuu kuwasaidia kuwachimbia kisima na kuwasambazia tenki za maji.
Wakaazi hao pia wamelalamikia ukosefu wa umeme katika eneo hilo akiiomba serikali kuwasaidia katika maswala hayo.