KAUNTI YA MARSABIT YALENGA KUHAKIKISHA SHERIA YA KUWALINDA WALEMAVU IMEBUNIWA KUFIKIA MWISHONI MWA MWAKA WA 2025.
December 3, 2024
NA GRACE GUMATO
Afisa anayesimamia chanjo ya Watoto kaunti ya Marsabit Abdub Boru amesema kuwa chanjo za watoto zilizoisha hapo awali sasa zimefika na zimeweza kusambazwa katika kaunti ndogo za North Horr, Laisamis na Moyale.
Akizungumza na idhaa hii afisini mwake Boru amesema idadi ya chanjo ya BCG iliyofika eneo bunge la Moyale ni 6,000, Laisamis 5000, Saku 4000 na North Horr ni 7,000, kwa ujumla ikiwa ni chanjo 22,000.
Chanjo ya kupitishia mdomo zilizofika eneo bunge la Moyale ni 4,000, Laisamis 3000, Saku 6000 na North Horr 2,000, jumla ikiwa 15,000.
Aidha chanjo ya Surua (Measles) zilizofika eneobunge la Moyale ni 4,000, Laisamis 3,000, Saku 5,000 na North Horr 3,000, kwa ujumla ikiwa ni 15,000.
Aidha Boru amesema kuwa chanjo ya HPV zinapatakana katika hospitali ya rufaa ya Marsabit akisema watoto wasichana kati ya umri wa maika 10–14 wanapaswa kupata chanjo hizo ambazo zinazuia saratani ya njia ya uzazi.
Hata hivyo Boru amewahimiza wakaazi wa Marsabit kupeleka watoto wao kupata chanjo ili kuepukana na maradhi