Local Bulletins

Wakaazi wa El Gadhe Wataka Viongozi Kuwasaidia Kusafirisha Chakula cha Msaada kilichokwama Maikona

PICHA: KWA HISANI
Na Isaac Waihenya
Wakaazi wa kijiji cha El-Ghadhe eneo bunge la NorthHorr wamewataka viongozi eneo hilo kuingilia kati na kuwasaidia kusafirisha chakula cha msaada ambacho wanasema kimekwama katika eneo la Maikona.
Wakizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu wakaazi hao walisema kuwa wamefahamishwa na DCC wa Maikona kupitia chifu wao kwamba chakula cha msaaada kutoka kwa serekali kuu tayari kimewasili katika eneo la Maikona hivyo kuwataka watafute namna kitakavyowafikia.
Wakiongozwa na Yattani Umuro wakaazi hao walitaja kwamba kwa sasa hawana uwezo wa kusafirisha chakula hicho huku akina mama wakitishia kutembea na wanao hadi Maikona na kuishi humo ili waweze kunufaika na chakula cha msaada.
Walisema kuwa siku za hivi maajuzi akina mama na wazee wamekuwa wakizimia kutokana na makali ya njaa na kuirai serekali ya kaunti, viongozi wao pamoja na mashirika yasiyokuwa ya kiserekali katika kaunti ya Marsabit kuwanusuru kabla hawajapoteza wapendwa wao.

Subscribe to eNewsletter