Local Bulletins

Vijana Marsabit Watolewa Wito Kuwa Mabalozi wa Amani

Mwenyekiti CDF Saku Guyo Bonaya

Na Adano Sharamo

Vijana hapa Marsabit wametolewa wito kuwa mabalozi wa amani na kuhubiri amani baina ya jamii mbalimbali ili kufikisha kikomo mizozo ya kikabila ambayo hushuhudiwa mara kwa mara katika kaunti ya Marsabit.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa hazina ya maendeleo ya maeneo bunge CDF katika eneo bunge la Saku Guyo Bonaya ni kwamba vijana ndio hutumika mno wakati wa mizozo kwa kuwa wanapatikana kiurahisi.

Akizungunza wakati wa uzinduzi wa mchezo wa soka utakaozileta timu tofauti kutoka eneo bunge la Saku katika shule ya msingi ya Karare, Bonaya alitaja kwamba Amani itapatikana kwa urahisi iwapo vijana watahusishwa kikamilifu katika safari ya kuisaka amani hiyo.

Bonaya alitaja kwamba vijana kutoka katika jamii tofauti watapata nafasi ya kutengamana pamoja kwani hafla hiyo ya michezo itaandaliwa katika lokesheni tofauti za eneo bunge la Saku.

Kauli yake imeungwa mkono na katibu katika hazina hiyo ya CDF Mwalimu Boru Athi ambaye alitaja kwamba zoezi hilo linalenga kuhakikisha kwamba kila mmoja kuanzia vijana katika kaunti ya Marsabit ni mabalozi wa amani.

Baadhi ya vijana waliohudhuria hafla hiyo wamepongeza hazina ya CDF na kukikariri kwamba wanafurahia kuweza kuunganishwa pamoja kwa jamii mbalimbali za Marsabit huku wakiwa na matarajio kuwa zoezi hilo litazidisha uiano na utengamano kwao.

Aidha vijana hao wamewachangamoto viongozi wa jimbo hili kuzidisha hafla kama hizo ili kuwaleta vijana pamoja mara kwa mara na kuimarisha utengamano.

Subscribe to eNewsletter