Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Ken Simiyu
Senator wa kaunti ya Turkana James Lomenen amelaani mauaji ya maafisa wanne pamoja na raia katika maeneo ya Kakong, barabara kuu ya kitale kuenda Lodwar.
Akiongea katika mji wa kainuk Turkanà kusini Lomenen ameilaumu serikali kwa upetepevu wao huku wananchi pamoja na walinda usalama wakiuliwa.
Hata hivyo ameongezea kwamba licha ya serikali kuwaahidi wananchi ulinzi pamoja na Mali yao bado wahalifu wanaendelea kuwaangamiza wasafiri.
Lomenen mwenye ghadhabu sasa ameiambia serikali kwamba iwapo wameshindwa kupambana na wahalifu warudishe silaha kwa Askari wa akiba ili waweze kujilinda wenyewe.
Kufikia sasa maafisa 4 na abiria 3 wameripotiwa kupoteza maisha yao. Viongozi wa vitengo vya usalama Turkana kusini wote kwa sasa wako hosipitali kupokea matibabu baada ya kupigwa katika makabiliano hayo na majangili.
Shughuli za usafiri katika barabara hiyo sasa zimepunguka maana madereva na wasafiri wanaofia usalama wao.