Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
Familia zinaomboleza vifo vya watoto watatu waliokufa maji katika mto wa Kathita kaunti ya Tharaka Nithi.
Watoto hao walikua wamekuenda kutafuta maji ya kufua sare zao wakati wa mkasa.
Kwa mujibu wa taarifa ni kwamba watoto hao walikuwa wanne wakati wa mkasa huo ila mmoja wao alifaulu kuogelea hadi ufuoni wakati wengine wakizidiwa na kusombwa.
Watoto hao wa umri wa miaka 13, 12 na miaka 10 walikuwa wametembea kilomita kadhaa kutafuta maji ili wafue nguo zao jana kwa ajili ya shule zinazofunguliwa kesho Jumatatu.
Chifu wa eneo hilo la Gituma, Kibaara Muthungu, amesema mmoja wa watoto hao alikuwa wa darasa la nane. Mtoto mmoja aliyeponea chupu chupu ndiye alipiga ripoti ila wakati wakaazi walipofika walipata kwamba tayari wameaga dunia.
Watoto wawili kati ya watatu walioaga dunia ni wa familia moja.