Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
By Radio Jangwani
Gharama ya maisha imesababisha watumiaji wa bidhaa kuanza kutumia bidhaa ya bei za chini ili kukidhi mahitaji yao ya kifedha.
Kulingana na utafiti wa kampuni ya geopol, watu wengi wamepunguza idadi ya bidhaa wanazotumia, wengine wakiacha kununua bidhaa ambazo si za dharura.
Wengi wamepunguza usafiri na kuanza kutumia njia za gharama za chini za uchukuzi.
Pia watu wengi wameanza kutumia fedha walizokuwa wakiwekeza katika akiba, na wengine kupunguza kiwango cha fedha katika akiba hizo, kuhamia makazi ya gharama ya chini, kuuza bidhaa za nyumbani na wengine wakitegemea mikopo.
Utafiti huo uliofanywa katika mataifa tisa ikiwemo Kenya, unaonyesha kuwa umekuwepo mfumuko wa bei za bidhaa hasa za matumizi ya nyumbani.
Miongoni mwa watu 400 waliojiwa humu nchini, asilimia 47 wanasema hawako katika hali mbaya zaidi ya kifedha kulinganishwa na miezi sita iliyopita huku asilimia 46 wakisema mapato yao yamepungua katika kipindi hicho.
Asilimia 88 imesema hali imekuwa mbaya zaidi, kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa na huduma mbalimbali za kimsingi, wakitaja kupanda kwa bei kwa bidhaa kama vile unga wa mahindi, mafuta ya kupikia, gesi ya kupikia, sukari na mbolea.
Kwa mujibu wa utafiti huo, asilia 90 ya wakenya wanasema kwamba viwango vya maisha yao vimeshuka mno kutokana na gharama ya juu ya maisha.