Local Bulletins

Viongozi katika kaunti ya Marsabit watakiwa kuongea kwa sauti moja.

Picha;Hisani

Na Silvio Nangori,

Kaunti ya Marsabit yaweza kushamiri amani endapo viongozi wa kisiasa wataongea kwa sauti moja.

Hayo ni kwa mujibu wa mwenyekiti wa Interfaith jimbo la Isiolo Ahmed Sett.

Ahmed Sett ambaye pia ni mweka hazina la baraza kuu la wazee nchini ametoa wito huo kwa viongozi wa kisiasa haswa katika kaunti ya Marsabit kuwa mfano bora kwa jamii za kauti hiyo.

Huku joto la kisiasa likiendelea kupanda hapa jimboni, wito umetolewa kwa kwa vijana Isiolo kutokubali kutumika kuzua vurugu kabla, wakati na hata baada ya uchaguzi mkuu.

Ahmed Sett anasema kwamba vijana wanajukumu la kulinda amani kwa kuwa katika msatari wa mbele kuhubiri amani hata kupitia mitadao ya kijamii

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter