Local Bulletins

Sunya Orre apuuzilia mbali hatua ya baraza la wazee la kirendile waliompendekeza John Lotoo Segelan kuwania ugavana kwa niaba ya jamii hiyo.

Mwaniaji wa kiti cha ugavana mwaka huu katika kaunti ya Marsabit Sunya Orre.
Picha;Hisani

Na Samwel Kosgei,

Mwaniaji wa kiti cha ugavana mwaka huu katika kaunti ya Marsabit Sunya Orre amepuuzilia mbali hatua ya baraza la wazee la kirendile waliompendekeza John Lotoo Segelan kuwania ugavana kwa niaba ya jamii hiyo.

Akizungumza na radio jangwani kwenye kipindi cha Bunge Letu, Orre amesema kuwa uamuzi wa wazee uliofanyika katika eneobunge la Laisamis majumaa kadhaa yaliyopita hautambuliki kwani tayari uamuzi wa kumbarikisha ulikuwa ushafanyika mwanzoni.

Aidha orre amekana madai kuwa jamii hiyo imegawanyika, badala yake akisema ni watu wachache tu ndio wanaotumiwa kuigawanya jamii na kueneza propaganda.

Anasema yuko tayari kuungana na john lotoo Segelan ili kupeleka jamii mbele na kufika kileleni. Anasema iwapo segelan hakuridhishwa na maamuzi wa jamii yuko tayari kufanya mchujo mwingine.

Wakti uo huo amesema lengo lake ni kubadilisha utawala wa jimbo hili kwa kuweka sera mwafaka zitakazosaidia wananchi. Ametoa wito kwa jamii yote ya Marsabit kukumbatia Amani suala analosema atahakikisha limepatikana kwa kushirikiana na serikali kuu.

Subscribe to eNewsletter