Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Na Machuki Dennson
Rais William Ruto amewafahamisha mawaziri wapya kuwa hawana budi ila kufaulu katika kazi zao kama mawaziri.
Rais amesema kuwa yuko tayari kufanya nao kazi kuhakikisha wanafaulu katika utendakazi kwa wakenya bila ya kufeli.
Amesema atawapa msaada wowote wanaohitaji ili kuwahudumia wakenya kama ilivyo katika katiba ya Kenya.
Akizungumza baada ya mawaziri wote kula kiapo rais amewakumbusha mawaziri kuwa wao ni mawaziri wa Kenya nzima na wala si maeneo wanakotoka.
Amesema anafahamu kuwa kuna misukumo kutoka maeneo wanatoka ila amewaonya kuwa kiapo chao ni kuhudumia taifa zima katika wizara yoyote watakayotumwa kuhudumu.
Ruto amewataka mawaziri kuwaheshimu viongozi waliochaguliwa kuwawakilisha wakenya katika utendakazi wao.
Ameweka wazi kuwa wajumbe watawawakilisha wakenya katika kuwauliza maswali na kufuatilia utendakazi wao kama mawaziri.
Kiongozi wa nchi amewakumbusha umuhimu wa kiapo ambacho wamekula leo kwamba ni muhimu Zaidi.