Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Na Silvio Nangori
Mtu mmoja ameaga dunia huku mwingine akinusurika na jeraha la risasi katika eneo la Merille kaunti hii ya Marsabit baada ya kuvamiwa na majambazi.
Akidhibitisha kisa hicho kamanda wa kaunti ndogo ya Laisamis Wyclif Lang’at amesema kwamba majambazi hao walimvamia marehemu ambaye ni mfanyibiashara mwendo wa saa tatu usiku wa kuamkia Jumanne na kumpiga risasi tumboni.
Majambazi hao walimwibia kiasi cha pesa ambacho bado hakijulikani.
Lang’at ameongeza kwamba majambazi hao walimpiga risasi mguuni mwanabodaboda mwengine walipokuwa wakitoroka.
Mfanyibiashara huyo aliaga dunia baada ya kufikishwa hospitalini Laisamis huku mwanaboda boda akiruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupokea matibabu.
Langat ametoa wito kwa wananchi kutoa habari iwapo kuna watu wanaowashuku kuhusika katika ujambazi huo.
Amesema kwamba maafisa wa polisi watakuwa wanashika doria katika maeneo hayo kuanzia saa moja usiku huku shughuli ya kuwasaka waliotekeleza uvamizi huo ukiendelea.