IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
Na Winnie Adelaide
Mshindi wa tuzo la Aster Guardian Global Nursing Award Ann Qabale Duba amerejea nyumbani na kazini kwake ambapo ametoa wito wa amani na utangamano.
Akizungumza jana baada ya hafla ya kumkaribisha nyumbani, Qabale amesema kuwa anajivunia ushindi huo na kulielekeza taji hilo kwa jamii nzima ya Marsabit huku akiitaka kuishi kwa Amani.
Amempogeza mwezake Jirma Bulle ambaye pia anatokea hapa jimboni Marsabit na kutaja kuwa kwa pamoja watajitolea kuwa mabalozi wa Amani jimboni na kuonyesha mfano unaofaa kuigwa na jamii za Marsabit.
Bi. Duba amesema atatumia fedha alizoshinda katika juhudi za kutetea usawa wa kijinsia, elimu ya mtoto wa kike jimboni sawa na kuimarisha mradi wake wa Kusaidia jamii chini ya wakfu wake wa Qabale Duba Foundation ili kuweza kuwafikia wengi wanaohitaji msaada.
Kadhalika amewataka wauguzi katika jimbo la Marsabit kujibiidisha na kutia fora katika kazi zao.